Fainali za Taifa za mashindano ya Miss Utalii Tanzania 2012/13, zilizo kuwa zimepangwa kufanyika 17,machi 2013  katika ukumbi wa Dar Live Dar es Salaam, zimesogezwa mbele hadi tarehe 30-3-2013,katika ukumbi utakao tangazwa badae. 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Rais wa Mashindano hayo nchini na Barani Afrika Erasto G., Chipungahelo, alisema kuwa sababu  ya kuahilishwa kwa fainali ni pamoja na upungufu wa bajeti ,uliosababishwa na baadhi ya wadhamini wakubwa walio ahidi kushindwa  kutimiza ahadi zao kama walivyo ahidi, hivyo kupelekea upungufu wa zaidi ya shilingi 170,000,000/= , kati ya bajeti ya shilingi 870,000,000/= zinazohitajika ili kukamilisha fainali hizo.
“Ili kulifanya shindano hili kwa ubora na kiwango cha kimataifa, tunahitaji sio chini ya shilingi 870 Milioni, ambapo hadi sasa tumefanikiwa kupata jumla ya shilingi 600Milioni, na tunaupungufu wa jumla ya shilingi 170 Milioni, ambao umesababishwa na baadhi ya wadhamini kushindwa kutimiza ahadi zao kulikotokana na matatizo mbalimbali waliyo yapata ya kibiashara. 
Mashindano haya kama yalivyo mashindano mengine nchini na Duniani yanategemea udhamini kutoka kwa sekta binafsi na za umma, kwani gharama za kuyaendesha na kuyaandaa mashindano haya ni kubwa,ambazo haziwezi kulipwa wala kufidiwa kwa kutegemea viingilio vya getini”.
Hali hii imetulazimu kuahilisha fainali hizi hadi 30-3-2013,ili kupata muda wa kupata kiasi hicho cha fedha, na kukamilisha maandalizi kwa ubora na viwango vya kimataifa. 
Taratibu za kupata fedha hizo zinakaribia kukamilika kabla ya tarehe ya shindano kutoka kwa wadau wa utalii katika sekta binafsi na za umma. 
Kambi ya washiriki inaendelea katika hoteli ya Ikondelelo Lodge Dar es Salaam, ambapo kuanzia jumanne tarehe 19-3-2013 , washiriki wote wakiambatana na waandishi wa habari, wataanza ziara ya wiki moja katika hifadhi za Taifa za Mikumi,Saadani na Udzungwa.
Wakiwa katika hifadhi ya taifa ya Udizungwa washiriki watapanda milima ya udizungwa hadi katika kilele cha Maporomoko ya maji ya Sanje , ambayo ni kivutio kikubwa katika hifadhi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. ukweli hapa gari za kitalii za kuwabeba hawa ma-miss zilikuwa ziwe 4 au 5 lakini kwa kuwa wote ni fimbo (wembambaa) na hawali kushiba basi gari hili 1 limewatosha. alexbura dar

    ReplyDelete
  2. RAIS WA KAMATI UMESEMA UNA DEFICITY YA 170 MIL., ALAFU BADO UNAONGEZA MATUMIZI KWA HIZO ZIARA AMBAZO KUTOKANA NA MAELEZO YAKO HAZIKUWEMO, SASA HUONI KAMA UNAJICHANGANYA ? NAFIKIRI KUNA SOMETHING ELSE !

    ReplyDelete
  3. si bora fedha hizo zikatumika kununua vitabu na vifaa vya elimu mashuleni kama madeski , au kuimarisha maji vijijini ambayo ni huduma muhimu? au nampigia zeze mbuzi?

    ReplyDelete
  4. haya mashindano toka mwanzo niliyaona ya kinjaa njaa na nikatoa maoni yangu lakini michuzi ukabana. Hawa mabinti toka niwaone wanavishwa hizo jezi za 100% polyster!! nimeona picha hapa wakishindania vipaji wana hizo polyster, wakitembelea mahali wana hizo jezi za polyster, wakienda mbuga za wanyama wana hizo jezi za polyster hivi hawasikii joto hawa? Kama kitu hakiwezekani kwa nini mna fosi??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...