MSANII mahiri wa muziki wa Injili kutoka Afrika Kusini, Sipho Makhabane ametunga wimbo maalum kwa ajili ya mashabiki wake wa Tanzania.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa amezungumza na msanii huyo na amemueleza kuwa amewaandalia zawadi Watanzania kwa ajili ya tamasha hilo.

“Sipho amefurahi sana kumualika kwenye tamasha letu, amenihakikishia licha ya nyimbo zake za kawaida, lakini pia atakuwa na wimbo maalum kwa Watanzania, amesema anawapenda Watanzania na ameandaa wimbo mzuri ambao ana uhakika mashabiki wataupenda.

“Mashabiki watakaokuja kwenye tamasha Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Machi 31 watapata fursa ya kumsikiliza msanii huyo pamoja na wimbo wake mpya ambao jina hakunambia lakini amesema ni zawadi nzuri kwa Watanzania,” alisema Msama na kuzitaja baadhi ya nyimbo za msanii huyo kuwa ni Moya Wami, Indonga, Akukhalwa, Over&Over, Nguy’zolo, Yizwa Nkosiseju, Hlalanami Nkosi Jesu, Yek’intokozo, Injabulo, Hlalanami Jesu, Makadunyiswe, Vuka Mphemlo, Mphefumlo na Moya Wami.

Kuhusiana na maandalizi mengine ya tamasha hilo alisema yanaenda vizuri na kwamba mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kwamba ni matumaini yake mashabiki watajitokeza kwa wingi.

Licha ya Sipho Makhabane, wasanii wengine wa nje ya Tanzania ambao tayari wamethibitisha kushiriki tamasha hilo ni , Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya na kwaya ya Ambassadors of Christ ya Kigali Rwanda inayotamba na albamu ya Mtegemee Yesu. Wasanii wa Tanzania waliothibitisha hadi sasa ni Rose Muhando, Upendo Nkone na John Lissu, kwaya ya Kinondoni Revival na kundi la Glorious Celebration.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...