Sign in to confirm you’re not a bot
This helps protect our community. Learn more
Yanga wamaliza kikao sakata dabi ya Kariakoo ,Arafat afunguka
Yanga wamaliza kikao,Arafat afunguka Mkutano wa Bodi ya Ligi Tanzania TPLB na viongozi wa Yanga umemalizika na Makamu wa Rais wa klabu hiyo ametoa neno kilichojiri ndani. Mkutano huo ambao ulianza saa 4:30 na kumalizika saa 6:53 mchana ukifanyika kwenye ofisi za Bodi hiyo zilizopo Ilala jijini Dar es Salaam. Akizungumza mara baada ya mkutano huo Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amesema klabu yao imeshiriki kikao hicho kuwasilisha msimamo wa wanachama na mashabiki wao. Akizungumzia juu ya kukubali kucheza mechi dhidi ya Simba Arafat amesema Yanga haikuwahi kusema kama itacheza mechi hiyo. "Tumemaliza mkutano na tulichofanya ni kuwasilisha msimamo wa klabu kutoka kwa wanachama na mashabiki wetu hilo ndio kubwa,"amesema Arafat Mara baada ya mujibu swali hilo Arafat aliondoka eneo hilo sambamba na viongozi wenzake. Afisa Habari wa Bodi ya Ligi Karim Boimanda amesema taarifa kamili juu ya mkutano huo itatolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi Almas Kasongo

Mwananchi Digital

1.16M subscribers
Chat Replay is disabled for this Premiere.