Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mgeni wake Mama Cherrie Blair wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, mara baada ya kufanya mazungumzo yao.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na mgeni wake Mama Cherrie Blair, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza walipokutana leo kwenye ofisi za WAMA tarehe 23.7.2013 Mama Blair yupo nchini akifuatana na mumewe Tonny Blair katika ziara ya kikazi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa nasaha zake baada kuwafuturisha viongozi wa serikali, madhehebu ya dini wa wilaya ya Mkuranga na wananchi wa kijiji cha Hoyoyo kilichoko karibu na Mkuranga katika Mkoa wa Pwani tarehe 23.7.2013.

Na Anna Nkinda - Maelezo

Viongozi wa dini nchini wametakiwa kuhubiri amani katika majukwaa yao ili jamii ielewe umuhimu wa kuwepo kwa amani na kuendelea kuishi kwa upendo na ushirikiano.

Wito huo umetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiwafuturisha wanakijiji cha Hoyoyo wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Mama Kikwete alisema kuwa viongozi wa dini wanajukumu kubwa la kuhakikisha kuwa waumini wao wanaelewa umuhimu wa amani katika nchi kwa kujenga mshikamano kama waasisi wa Tanzania walivyouanzisha .

“Katika shughuli yetu hii tumekusanyika watu wa dini mbalimbali wanaofunga mwezi huu na wengine mwezi mwingine lakini dua ni dua kupitia kwa mwanadamu yeyote Mwenyezi Mungu inamfikia, hivyo basi tuzidi kushikamana kwa kila jambo”.

Aliendelea kusema kuwa amani inatafutwa kwa miaka mingi lakini inaweza kutoweka kwa muda mchache hivyo basi kila mtu hasa viongozi wa dini watumie muda wao kuhubiri umuhimu wa amani katika nchi na neno amani lisitoweke ndani ya vinywa vyao.

Kwa upande wake Sheikhe Athuman Kinyozi alimshukuru Mama Kikwete kwa futari aliyoiandaa kwa ajili yao na kusema kuwa mtu anayejitoa kwa ajili ya kufuturisha wengine anapata thawabu kwa Mwenyezi Mungu.

Sheikhe Kinyozi alisema kuwa kufanya kitendo cha kufuturisha si lazima uwe na uwezo mkubwa kifedha bali unaweza ukanunua hata tende au maji na kuwapa watu waliofunga kile ulichowapa kikiwa ni kitu cha kwanza kutia midomoni mwao utalipwa thawabu za funga ya wale wote uliowapa kitu walichokula.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 24, 2013

    Ankal Michuzi mie naomba uwe una recodi hizi speech na kutuwekea humu ili tulio mbaali tusikilize wanaongea kitu gani. Ni waazo tu jamani. Ramadhani Kareem.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 24, 2013

    SAWA KABISA MTOA MAONI WA KWANZA, KWANI SISI HUA TUNAONA PICHA TU HAYUJUI WANAONGELEA NINI NI MUHIMU NA SISIS TULIO NJE YA NCHI TUWE YUNASIKIA NINI WANACHO ZOZR ILI TUWEZE KUCHANGIA MAWAZO

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 25, 2013

    siyo mlio nje ya nchi tu,maana hata sisi tulio humu ndani hatujui wameongelea nn na pia hizi ziara za hawa viongozi waliotoka madaraka wanaokuja kutembelea huku kwetu pia ni vyema tukawasikia wanazungumza nn maana twahisi kama tunauzwa vile bila taarifa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...