Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Barack Obama wakipokea saluti wakati nyimbo za Taifa zikipigwa wakati wa kuondoka kwa Rais huyo wa Marekani leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Nyuma yao ni Mama Salma Kikwete na Mama Michelle Obama pamoja na Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange pamoja na IGP Saidi Mwema . Kushoto ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage na Mkuu wa Itifaki wa Ikulu ya Marekani (White House) Balozi Capricia Marshall. Ziara ya Rais Obama nchini imetajwa kuwa moja ya ziara za viongozi wa nje zilizofanikiwa sana, ambapo maelfu ya Watanzania walijitokeza kumlaki na kumuaga.
 Rais Barack Obama akiagana na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam huku Mstahiki Meya wa Ilala pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula wakisubiri zamu zao
 Rais Obama na mkewe wakikwea pipa lao la Air Force One
 Rais Obama na mkewe wakipunga mikono kuaga Watanzania
 Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiaga wageni wao
Rais Kikwete, Mama Salma Kikwete, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Adam Malima (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe  Alfonso Lenhardt wakipungia kuaga wageni wao. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...