Viongozi wa dini za Kikristo na Kiislam wametakiwa kutumia vema nyadhifa na fursa walizonazo katika kuhakikisha kuwa waamini wao wanadumisha Amani na Utulivu Nchini ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha waumini wao bila kujali mipasuko mbalimbali inayojitokeza hapa nchini.

Wito huo Umetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe Bernard Membe baada ya Misa iliyoambatana na uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa hosteli ya kanisa katoliki parokia ya Nachingwea sambamba na uzinduzi wa Kitabu cha maandiko ya sehemu ya bibilia iliyotafsiliwa kwa lugha ya kabila la Kimwera.

Mhe Membe alibainisha kuwa hali inayojitokeza hivi sasa inaweza kukomeshwa iwapo viongozi wa dini watakuwa msitari wa mbele kuwaelimisha waumini wao madhara ya ukosefu wa amani na Kutokubali kurubuniwa na kuwa vyanzo vya uvunjifu wa amani.

Awali akisoma taarifa ya Umoja wa Makanisa ya kikristo Nachingwea,Mchungaji wa EAGT,Pius Mnombela alieleza kuwa Umoja huo umefanikiwa kutafsiri vitabu vyote vya agano jipya ambapo vitabu vya Injili ya Luka na Marko vimefanyiwa ukaguzi wa awali na kubainisha lengo la kuanzisha Mpango wa Kuanzisha Utafsri huo na uzinduzi wa kitabu cha Biblia kwa Lugha Asili ya Kimwera .
 Naye Fr Ngombo wa kanisa hilo aliwataka waumini kuchangia Parokia zao kufuatia Makanisa Mengi kukosa wafadhili wa Nje ambapo katika Harambee Iliyoendeshwa na Waziri Membe na kufanikisha kuchangiwa kiasi cha shilingi milioni 31 kati ya fedha hizo Waziri huyo alichangia shilingi milioni 10 pia aliahidi kuhakikisha Jengo hilo linakamilika kama lilivyokusudiwa kufuatia Nguvu kubwa zilizoonyeshwa na waumini mbalimbali
Uzinduzi huo wa Biblia ya Kimwera,Uwekaji wa Jiwe la Msingi na Harambee ya kukamilisha ujenzi wa Hostel ya Parokia hiyo umefanikiwa kushirikisha makundi mbalimbali bila kujali Itikadi zao za imani na udhehebu na kuwezesha kupata Tafsiri sahihi ya Biblia kwa Lugha ya Kimwera lugha ambayo utumika na wakazi wengi wa Wilaya za Ruangwa,Lindi na Nachingwea Mkoani LINDI

Moja ya kurasa za kitabu cha maandiko ya sehemu ya bibilia iliyotafsiliwa kwa lugha ya kabila la Kimwera.
Mhe Bernard Membe akizindua Kitabu cha maandiko ya sehemu ya bibilia iliyotafsiliwa kwa lugha ya kabila la Kimwera.
Vifijo baada ya uzinduzi wa kitabu hicho
Fr. Ng'ombo akiongea wakati wa hafla hiyo
Mhe Membe akifunua pazia kama ishara ya kuweka  jiwe la msingi la ujenzi wa hosteli ya kanisa katoliki parokia ya Nachingwea
Kanisa Katoliki parokia ya Nachingwea kwa nje
Mhe Bernard Member akihutubia waumini
Mhe Bernard Membe akiwa kanisani humo
Waumini wakiwa katika misa hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 11, 2013

    Kasusula ni msaidizi wa Membe siku hizi?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 11, 2013

    Hiyo ndio itakua lugha ya taifa kusini?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 11, 2013

    Mmmh kazi ipo!Ila baba alikua hapendi mchezo huu....bahati yenu hayupo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...