Balozi wa Japan nchini Tanzania, Bw. Masaki Okada (kushoto) akifurahia jambo na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe(mwenye suti nyeusi) ndani ya Behewa la Treni ya Dar es Salaam leo asubuhi, wakati Balozi huyo alipotembelea Shirika la Reli Tanzania(TRL) na pia kutembelea eneo la reli lililoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Harrison Mwakyembe akipanda kwenye kiberenge kuelekea kwenye eneo la Tabata Mwananchi lililoharibiwa na mvua kubwa zinazoendela kunyesha jijini Dar es Salaam. Waziri wa Uchukuzi na Balozi wa Japan nchini Tanzania walitembelea eneo hilo leo asubuhi kuangalia maendeleo ya ujenzi wa eneo hilo. Nyuma ya Waziri Mwakyembe ni Balozi wa Japan Nchini Tanzania, Masaki Okada.
Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Harrison Mwakyembe,akitoa ufafanuzi wa uharibifu uliotokea kwa Balozi wa Japan Nchiini Tanzania,Bw. Masaki Okada, leo asubuhi walipotembea eneo hilo.
Balozi wa Japan nchini Tanzania,Bw. Masaki Okada akishuka kwenye kiberenge, mara baada ya kumaliza ziara ya kuangalia eneo lilihoribiwa na Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam na kusababisha usafiri wa treni ya Dar es Salaam kusimama. Balozi huyo alitembealea eneo hilo leo asubuhi akiongozana na Waziri wa Uchukuzi,Dkt Harrison Mwakyembe.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), Dkt. Damas Ndumbaro(Kulia) anaemaliza muda wake , akitoa maelezo kwa Balozi wa Japan Tanzania, Bw. Masaki Okada (mwenye tai ya njano) na Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Harrison Mwakyembe(kulia), wakati Balozi huyo na Waziri wa Uchukuzi walipofanya ziara kujionea maendeleo ya usafiri wa Treni kwa Upande wa TAZARAleo asubuhi.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) anaemaliza muda wake, Dkt. Damas Ndumbaro(Kulia), akitoa ufafanuzi wa ratiba ya treni ya TAZARA inayofanya safari zake kutokea Stesheni ya TAZARA kwenda Mwakanga , kwa Balozi wa Japan nchini Tanzania (mwenye tai ya njano), wakati alipotembelea Stesheni hiyo leo asubuhi.Balozi huyo aliongozana na Waziri Mwakyembe katika ziara hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...