Sign in to confirm you’re not a bot
This helps protect our community. Learn more
MAT YAITAKA SERIKALI KUJA NA SULUHISHO AJIRA ZA MADAKTARI, UBORA WA HUDUMA
Mkutano wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) umekuja na maazimio manne ya kisera, ikiwemo kuitaka Serikali kuongeza kasi ya kuajiri wataalamu wa afya, bajeti ya kushughulikia afya, ubora wa huduma na kinga dhidi ya magonjwa. Kwa mujibu wa MAT, Serikali imetumia fedha nyingi kufanya uwekezaji wa wataalamu na kwa sasa wapo wa kutosha, lakini tatizo ni namna watakavyoitendea kazi taaluma waliyoisomea. Maazimio hayo yametolewa leo Ijumaa, Juni 20, 2025 wakati wa kufungwa kwa Kongamano la Kitaifa la Tiba na Maadhimisho ya miaka 60 ya MAT. Akitoa maazimio hayo, Rais wa MAT, Dk Mugisha Nkoronko amesema nchi haiwezi kuwa na ubora wa huduma, ikiwa na vituo vingi vinavyowekwa bila kuwa na watoa huduma za afya. Amesema katika sekta ya afya kuna upungufu wa zaidi ya asilimia 55, na katika hilo wote wanawajibika kwa pamoja kuona namna gani upungufu huo utazibwa. Video na Khatibu Mgeja.

Mwananchi Digital

1.16M subscribers
Chat Replay is disabled for this Premiere.