Sign in to confirm you’re not a bot
This helps protect our community. Learn more
" HALMASHAURI WASICHUKUE VISHIKWAMBI WALIVYOKUA WANATUMIA MADIWANI WANAOMALOZA MUDA" MCHENGERWA.
206Likes
26,765Views
Jun 202025
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa, amemwangiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo Adolf Ndunguru kuwaandikia wakurugenzi wa Halmashauri kutokuchukua vishikwambi walivyokuwa wanatumia madiwani waliomaliza muda wao pamoja na stahiki zao. Akizungumza kwa njia ya simu leo 20 Juni, 2025, baada ya kupigiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda, Waziri Mchengerwa amesema kuwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia yametekelezwa vyema kupitia usimamizi madhubuti wa Mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. "Ni kazi ya nguvu, jasho, ubunifu na stadi za madiwani kote nchini. Nawapongeza Mameya wote kwa kazi yao kubwa, hususan Meya wa Jiji la Arusha. Kazi yao imeandikwa katika kitabu cha dhahabu kwa kuwa wamewahudumia wananchi wanyonge kwa moyo wa uzalendo," amesema Mhe. Mchengerwa. Katika hatua nyingine, Waziri Mchengerwa ametumia nafasi hiyo kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Makonda, kwa kazi kubwa na yenye mafanikio anayoifanya mkoani humo, akisema kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI inatambua na kuthamini jitihada zake. Maelekezo hayo yametolewa rasmi kwa mabaraza yote ya madiwani nchini, yakisisitiza dhamira ya serikali kuimarisha mazingira ya kazi kwa viongozi wa ngazi za msingi katika mfumo wa utawala wa nchi.

Millard Ayo

5.74M subscribers