Sign in to confirm you’re not a bot
This helps protect our community. Learn more
KUKOSEKANA ELIMU MATUMIZI VIFURUSHI VYA BIMA KUNAVYOWATESA WATANZANIA
Taasisi ya Utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR) imesema changamoto ambayo wananchi wanapata baada ya kupata bima za afya ni kushindwa kujua matumizi sahihi ya vifurushi vya bima. Imesema hali hiyo imekuwa ikisababisha wengi wao kujikuta wakienda katika vituo vya ngazi za juu za matibabu, hivyo kupewa dawa za mnyororo wa juu hali inayosababisha kuzikosa baadaye wanapoenda vituo vya afya vya ngazi ya chini. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Taarifa za Tafiti, Nimr na Mtafiti Mwandamizi, Dk Mary Mayige wakati wa kongamano la Kitaifa la Tiba linalokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 60 ya Chama cha Madaktari Tanzania, MAT. Amesema ni muhimu wananchi wafuate mnyororo wa rufaa ili kuongeza ufanisi wa huduma wanazozitoa madaktari, kwani wengi akishapata bima anakwenda ngazi za juu za huduma. Mayige ameshauri wananchi wafuate ngazi za rufaa ili kupunguza changamoto hiyo. Aidha katika hatua nyingine, Dk Mayige ameitaka jamii kuhakikisha inapima afya mara kwa mara ili kujiepusha na magonjwa yasiyoambukiza ambayo hayana dalili.

Mwananchi Digital

1.16M subscribers
Chat Replay is disabled for this Premiere.