Sign in to confirm you’re not a bot
This helps protect our community. Learn more
UJUMBE WA SHEIKH PONDA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025
Dar es Salaam. Shura ya Maimamu Tanzania imemuomba Rais Samia Suluhu Hassan akutane na wadau wanaowakilisha wananchi ili kujadili malalamiko yaliyopo kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa Oktoba mwaka huu. Kauli hiyo imetolewa leo, Juni 7, 2025, na Katibu wa Shura hiyo, Sheikh Issa Ponda, wakati akiwasilisha waraka maalumu wa Shura kwenye Baraza la Iddi Adh-ha, uliobeba mapendekezo kuhusu namna bora ya kuendesha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Sheikh Ponda amesema kuwa sheria za uchaguzi ni msingi muhimu wa demokrasia na haki, lakini zimeendelea kulalamikiwa na wananchi pamoja na taasisi mbalimbali. Aidha, Shura ya Maimamu imeitaka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kusimamia mchakato huo kwa haki na kuhakikisha kuwa hakuna mwananchi ananyimwa haki ya kupiga kura au kuchaguliwa kwa sababu ya makosa madogo. Video imeandaliwa na Khatibu Mgeja.

Mwananchi Digital

1.16M subscribers
Chat Replay is disabled for this Premiere.