Baraza la Wazee wa Chadema (Bazecha) limesema kuwa licha ya kuondoka kwa baadhi ya viongozi na wanachama, chama hicho kimezidi kuwa imara kuliko wakati mwingine wowote.
Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa Mei 16, 2025 na Mwenyekiti wa Bazecha Kanda ya Pwani, James Haule, akieleza kuwa mabadiliko yanayojitokeza ndani ya Chadema ni sehemu ya safari ya kisiasa, akifananisha hali hiyo na 'bahari inayotema uchafu'.
"Baraza la Wazee baada ya kufuatilia tumegundua chama kipo imara kuliko wakati mwingine wowote. Bahari inatema uchafu. Hivyo, nitoe wito kuwa anayeshuka kwenye basi amefika mwisho wa safari. Siasa ni safari ndefu; wanaoshuka huenda wasifike nchi ya ahadi wanayotamani," amesema Haule.
Chadema kwa sasa inaendesha kampeni ya 'No Reforms, No Election' chini ya Mwenyekiti wake Tundu Lissu, ikisisitiza kufanyika kwa marekebisho ya sheria za uchaguzi kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.
Video na Ally Mlanzi ā¦...more
...more
Show less