Sign in to confirm you’re not a bot
This helps protect our community. Learn more
WADAU WATAKA SEKTA BUNIFU KUPEWA KIPAUMBELE NA SEKTA YA HABARI
0Likes
28Views
May 122025
Wadau wa masuala ya ubunifu wamevitaka vyombo vya habari nchini kuongezwa kwa kasi ya uandishi wa habari za ubunifu kwa sababu ndiyo dunia inakokwenda. Ili kufanikisha hilo, wametaka waandishi wa habari kujengewa uwezo ili waweze kuwa wabobezi wa eneo hilo ili kuondoa ombwe lililopo sasa la watu kuandika vitu wasivyovifahamu kwa undani. Hayo yamesemwa leo Mei 12, 2025 katika ufunguzi wa wiki ya ubunifu (Innovation week) ambapo wadau wa vyombo vya habari na wabunifu walijadili kwa pamoja jukumu la vyombo vya habari katika kuendeleza ubunifu na ujasiriamali kama ajira kwa vijana. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Simplitech, Baraka Cassian amesema bado vyombo vya habari havijui namna bora ya kuandika habari za kampuni changa kwa sababu hawajui vyema ni kitu gani hasa. β€œNa hata wanapoandika wanajikuta wanatafuta namna ya kuandika kitu ili kifanye vyema mtandaoni badala ya kuzifanya zieleweke vyema kwenye jamii,” amesema Cassian. Mbali na vyombo vya habari amesema hata vijana wenyewe wanapokuja na hizo kampuni change wanakuwa hawajui kuwa ni kitu kinachoweza kuwakuza kiuchumi. β€œBado vijana wengi wanakosa namna itakayowawezesha kujua namna bunifu zao zinavyoweza kugeuzwa kuwa biashara na kufaidika nazo. Hivyo vyombo vya habari vinapaswa kuwekeza kwenye kuonyesha kwa upande wa kibiashara ili kuwavutia vijana wengine kuingia huko,” amesema Cassian. Mwanzilishi wa kampuni ya Waga, Gibson Kawango amesema kuwepo kwa pengo la uelewa kati ya waandishi wa habari imekuwa ikiwafanya washindwe kuuliza maswali magumu yanayoweza kuleta uelewa kwa jamii. Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited (MCL), Rosalynn Mndolwa-Mworia amesema huu ndiyo wakati wa sekta ya habari ya Tanzania kuchukua nafasi yake kikamilifu kama chombo cha mabadiliko ili kuhakikisha habari hizo zinaandikwa kwa wingi.

Mwananchi Digital

1.16M subscribers