Sign in to confirm you’re not a bot
This helps protect our community. Learn more
CHOMBO CHA KUSIMAMIA MIUNDOMBINU YA MICHEZO KUANZISHWA
0Likes
129Views
May 72025
Chombo cha kusimamia miundombinu ya michezo kuanzishwa Serikali imeanza mchakato wa kuanzisha chombo maalumu cha usimamizi wa miundombinu ya michezo katika kukabiliana na changamoto za uendeshaji na matunzo yake. Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi leo Mei 7,2025 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 2025/26. Profesa Kabudi amesema chombo hicho kitakuwa na mamlaka ya kusimamia uendeshaji, ukarabati na matunzo ya miundombinu yote ya michezo nchini. “Hivyo, ni matumaini yetu kwamba kuwapo kwa chombo hiki kutapunguza changamoto za usimamizi wa miundombinu na kutaongeza thamani ya miundombinu ya michezo nchini,”amesema Profesa Kabudi.

Mwananchi Digital

1.16M subscribers