Sign in to confirm you’re not a bot
This helps protect our community. Learn more
WALIOUA WALINZI WA SUMA JKT CRDB ,DCB KUNYONGWA
Dar es Salaam. Mahakama Kuu, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imewahukumu adhabu ya kifo, watu wawili waliovamia Benki mbili za CRDB na Benki ya Biashara ya DCB za jijini Dar es Salaam na kuua watu watatu kwa mtutu wa bunduki. Tukio hilo la mauaji lilitokea saa 8:40 mchana wa Desemba 8, 2015 katika eneo la Chanika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wakati wa uvamizi wa benki hizo ambapo miongoni mwa waliouawa ni walinzi wawili wa Suma-JKT. Waliouawa wametajwa kuwa ni Ramadhan Rashid Halili na Shani Rajabu Mohamed waliokuwa walinzi wa Suma JKT katika Benki ya CRDB na mtu mwingine ambaye ametajwa kuwa ni Gabriel John Ngwangai. Ingawa hukumu inawataja waliohukumiwa ni washitakiwa ambao ni Mohamed Hassan na Rajabu Ally, lakini Katibu Mkuu wa Shura hiyo, Sheikh Ponda Issa Ponda, kupitia ukurasa wake wa X (Twitter) amewatambulisha watu hao kuwa masheikh. Hukumu hiyo imetolewa Aprili 28, 2025 na Jaji Butamo Phillip na nakala ya hukumu hiyo kuwekwa katika tovuti ya Mahakama leo Aprili 30, 2025 ambapo Jaji alimwachia huru mshitakiwa wa tatu, Kulwa Athman kwa kukosekana ushahidi. Usikilizwaji wa kesi hiyo uliendeshwa pasipo kutaja majina ya washitakiwa wala anuani za makazi ambapo mashahidi wa upande wa Jamhuri walitambulishwa mahakamani kwa namba P25,P43,P22,P7,P27,P20, P23 na namba P24. Mbali na kutotajwa majina na anuani za makazi yao, lakini mashahidi hao walitoa ushahidi wao wakiwa wamefichwa katika kizimba maalumu kilichowekwa mahakamani ili kutoonekana ili kutotoa utambulisho wao halisi wa sura. Ushahidi ulivyokuwa Shahidi wa kwanza wa Jamhuri, alieleza kuwa mwaka 2016 alikuwa miongoni mwa maofisa waliokuwa katika kikosi kazi kilichoundwa kwa ajili ya kufanya upelelezi wa matukio ya ugaidi, ambayo yalihusisha uvamizi wa benki hizo mbili. Kulingana na shahidi huyo, marehemu katika shauri hilo waliuawa wakati wa uvamizi wa benki hizo ambazo zinatizamana, ushahidi ambao uliungwa mkono na shahidi wa pili wa Jamhuri ambaye alikuwa Ofisa Mfawidhi wa Benki ya CRDB. Shahidi huyo alieleza kuwa benki hiyo ilikuwa na walinzi wawili wa Suma JKT, mmoja mwanamke na mwingine mwanaume ambapo mlinzi mwanamke alipangiwa ndani ya benki na mwanamme alipangiwa nje akiwa na bunduki. Alieleza kuwa Desemba 8, 2015 saa 7:40 mchana, benki yao ilivamiwa na watu wenye silaha ambapo wakati huo alikuwa anapata chakula cha mchana karibu na ofisi yake, na wakati anasubiri aletewe chakula, alisikia milio ya risasi. Milio hiyo ilikuwa inatokea uelekeo wa benki yake ambapo alikimbilia Kituo cha Polisi Chanika kutoa taarifa na alimkuta Ofisa wa Polisi ambaye alimfahamisha kuwa na yeye amesikia milio hiyo na ametoa taarifa kituo cha Stakishari. Baada ya kutoa taarifa hiyo, waliongozana na Ofisa huyo wa Polisi hadi benki na alipofika alikuta wafanyakazi wenzake wakiwa nje wanalia na waliwaeleza kuwa walinzi wote wawili wameuawa na akamuona Ramadhan akiwa amelala sakafuni. Alikuwa amekufa na alikuwa na matone ya damu chini ya kifua na baadae akamuona mlinzi mwingine, Shani akiwa na majeraha kichwani akiwa naye amelala sakafuni lakini naye alikuwa tayari ameshapoteza maisha.

Mwananchi Digital

1.16M subscribers
Chat Replay is disabled for this Premiere.