Sign in to confirm you’re not a bot
This helps protect our community. Learn more
BITEKO ALETA KICHEKO KWA WATANZANIA GHARAMA ZA UMEME KUPITIWA UPYA NCHINI
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amesema Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeanza kufanya tafiti ya gharama za huduma ya umeme nchi nzima. Amesema kwa sasa bei ya kuunganisha umeme vijiini kote ni Sh27,000, Kwa maeneo ambayo ni Vijiji- miji, Serikali inaendelea kuunganisha umeme kupitia mpango mahsusi wa Taifa wa Nishati. “Kwa mwaka wa fedha 2025/26, Serikali kupitia REA (Wakala wa Nishati Vijijini) imetenga Sh40 bilioni ili kuanza kuunganisha umeme kwa bei ya Sh27,000 katika maeneo mbalimbali yenye sura ya vijiji miji,”amesema. Amesema Serikali imekuwa ikitoa ruzuku ya wastani wa asilimia 58 ya gharama za kuunganisha umeme katika maeneo ya mjini ambapo gharama halisi ni sh546,764 lakini mwananchi hulipa Sh 320,960. Video na Hamis Mniha

Mwananchi Digital

1.16M subscribers
Chat Replay is disabled for this Premiere.