Sign in to confirm you’re not a bot
This helps protect our community. Learn more
SERIKALI KUANZA KUNUNUA MAHINDI MEI, WAKULIMA WATAKIWA KUZINGATIA USAFI WA BIDHAA
2Likes
337Views
Apr 142025
Dodoma. Serikali imewataka wananchi wa Ngara kujiandaa, kwani mwezi ujao (Mei) itaanza kununua mahindi waliyozalisha, lakini ikatoa tahadhari kuhusu usafi wa mahindi hayo. Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde, ameliambia Bunge leo Jumatatu, Aprili 14, 2025, wakati akijibu swali la mbunge wa Ngara, Ndaisaba Ruhoro, aliyeuliza ni lini Serikali itaanza kununua mahindi ya wananchi wa Jimbo la Ngara kupitia NFRA. Naibu Waziri amesema zoezi la ununuzi wa mahindi, ikiwemo Jimbo la Ngara, linatarajiwa kuanza Mei 2025, baada ya Serikali kukamilisha maandalizi yote ya shughuli hiyo. Amesema wakulima wanasisitizwa kuzingatia usafi wa mahindi na kuhakikisha mahindi yao yamekaushwa hadi kufikia kiwango cha unyevu wa asilimia 13.5, ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza endapo mahindi yao hayatakidhi ubora unaohitajika. Video na Hamis Mniha.

Mwananchi Digital

1.16M subscribers