Sign in to confirm you’re not a bot
This helps protect our community. Learn more
MWANAMKE AFARIKI AKIWA ‘GUEST HOUSE’, ALIINGIA NA MWANAUME, POLISI WASEMA WALIKUTA POMBE, CHIPSI
Mwanza. Mwanamke mmoja ambaye bado hajafahamika, amekutwa amefariki dunia katika chumba cha nyumba ya wageni (guest house) eneo la Usagara Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza. Taarifa ya Kamanda wa Polisi, Wilbrod Mutafungwa iyotolewa jioni ya Machi 19, 2025 imesema mwanamke huyo alikutwa amefariki kwenye chumba namba tatu katika guest hiyo inayojulika kwa jina la First and Last guest. Mutafungwa amesema baada jeshi hilo kufika katika eneo la tukio jana, walibaini Machi 18, 2025 saa 1 jioni alifika mgeni katika nyumba hiyo aliyejiandikisha kwa jina la Bilal William, mkazi wa Geita akitokea Chato kuelekea Nzega mkoani Tabora. Amesema mgeni huyo alipewa chumba namba tatu na kuweka mizigo yake, ilipofika saa nne usiku alitoka chumbani akidai anakwenda kutafuta chakula, na ilipofika usiku mkubwa mwanaume huyo alirudi katika nyumba hiyo ya kulala wageni akiwa na mwanamke. “Inadaiwa kuwa ilipofika saa 12:00 asubuhi wakati wahudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni wakihitaji kufanya usafi ndipo walipokuta mlango wa chumba hicho ukiwa na komeo lililofungwa kwa nje hali hiyo iliwatia mashaka hivyo kufungua kufuli hilo na kuingia ndani, na ndipo walipooana kuna mwanamke asiyefahamika kwa jina amefungwa usoni kwa kitambaa pamoja na mikwaruzo usoni mwake huku akiwa uchi na mwanaume akiwa haonekani,”amesema Mutafungwa Amesema mwili wa marehemu umepelekwa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi kwa ajili wa uchunguzi licha ya kuwa bado haujatambulika hadi sasa. Imeandikwa na Mgongo Kaitira.

Mwananchi Digital

1.16M subscribers
Chat Replay is disabled for this Premiere.