Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inamshikilia Stanley Bulaya, mkazi wa Kata ya Nguruka, wilayani Uvinza, Mkoa wa Kigoma kwa tuhuma za kumteka mtoto wa kiume (8) mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mbezi ya jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo la utekaji lilifanyika Machi 6, 2025 eneo la Mbezi Luis, Wilaya ya Ubungo, mtoto huyo alipokuwa anaelekea shuleni baada ya kushushwa na baba yake mzazi kwenye kituo cha daladala jirani na anaposoma.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Jumapili Machi 9, 2025 Kamanda wa kanda hiyo, Jumanne Muliro amesema siku hiyo mtoto hakurudi nyumbani hadi saa moja jioni wazazi wake walipoanza kumtafuta huku wakiwasiliana na mwalimu aliyepigiwa simu na mtuhumiwa kutaka namba za wazazi. âŚ...more
...more
Show less