Sign in to confirm you’re not a bot
This helps protect our community. Learn more
HOTUBA YA RAIS ZELENSKYY KWA KISWAHILI, AMUHOFIA PUTIN, ALILIA JESHI LA ULAYA
Jana Jumamosi Februari 15,2025, viongozi wa mataifa mbalimbali duniani wakiwemo Marais walikutana Jijini Ujerumani kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali likiwemo suala la mtikisiko wa kiuchumi unaochochewa na kutetereka kwa hali ya kiusalama ulimwenguni. Miongoni mwa waliohudhuria, ni Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ambaye lengo lake kubwa ilikuwa ni kupata msimamo wa Marekani juu ya hatma ya taifa hilo kuifadhiri Ukraine silaha ma vifaa vitakavyowezesha kuendeleza mapigano dhidi ya vikosi vya Rais Vladimir Putin wa Russia. Hata hivyo, Makamu wa Rais wa Marekani, JD Vance ya kuwa Marekani haitokuwa na sehemu hata chembe ya kutoa misaada ya kijeshi kwa Ukraine na mataifa ya Ulaya kwa kile alichodai taifa lake chini ya uongozi wa Rais Donald Trump linawekeza nguvu kwenye ukuzaji wa uchumi wa raia wa taifa hilo na si nje ya taifa hilo. Majibu hayo ya JD Vance, yanaonekana kutomfurahisha Rais Zelemskyy ambaye alionekana kuwa na matumaini kibao kuwa huenda Marekani ingekuja na msimamo wa kuishawishi Jumuiya ya Kujilinda ya NATO kuridhia Ukraine kuwa mwanachama. Pia aliamini kupitia jukwaa hilo Marekani itatangaza hadharani kuwa sasa ufadhiri wa silaha zake na wanajeshi utaelekezwa nchini Ukraine. Hata hivyo, JD Vance aliibua hoja ya kuyataka mataifa ya Umoja wa Ulaya kutumia bajeti kubwa kujiimarisha kijeshi na kiuchumi ili yaache kuitegemea Marekani linapofika suala la vita kwa kile alichodai kuwa hali itabadilika kuanzia sasa kwemye suala la kuitegemea Marekani kiusalama. Katika kuonyesha kutofurahishwa na hotuba ama mazungumzo yake na JD Vance, Zelenskyy aliibuka na kuitaka EU (Jumuiya ya Ulaya) kuunda jeshi lake la pamoja ili kukabiliana na Jeshi la Russia kwa kile ambacho amedai Russia inajipanga kuanzisha mashambulizi dhidi ya mataifa ya ulaya baada ya kuimaliza Ukraine. Nimekusogezea hotuba ya Rais, Volodymyr Zelenskyy kwa kiswahili juu ya kile alichozungumza mbele ya viongozi hao wa mataifa ya Ulaya. Imeandikwa na Mgongo Kaitira.

Mwananchi Digital

1.16M subscribers
Chat Replay is disabled for this Premiere.