Miss utalii Tanzania 2013, Hadija Mswaga (kushoto) akiingia kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana, kuelekea Equatorial Guinea kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia ya Miss Tourisim World 2013, pembeni ni mshindi wa tatu, Teresia Kimolo. aliyemsindikiza (Picha na Hosea Joseph)


BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata), limempa karipio kali Mwenyekiti wa shindano la Miss Utalii, Gideon Chipungahelo kwa kosa la kudhalilisha baadhi ya washiriki na malalamiko kufanyiwa kazi na Baraza hilo.


Karipio hilo lilitolewa baada ya Basata kupitia tathmini iliyohusisha vipande vya matukio yaliyorekodiwa (clips) na kujionea namna wasichana wanavyofanyiwa vitendo vya udhalilishaji na Chipungahelo kwa kipindi cha  kambi ya miezi mitatu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Haya ni makosa ya jinai ashtakiwe!

    ReplyDelete
  2. Inasikitisha sana maana kama huyo bint hakustahiki kuchukua taji hilo ni dhahiri huko aendako hatafanya vizuri na tunaharibu jina la nchi yetu.

    Kikubwa zaidi ya nilicho kieleza hapo juu ni udhalilishaji wa binti zetu kwa namna ambayo wanajikuta wanaingia katika mitego ya ngono bila ridhaa kwa watu ambao hata afya zao ni mgogoro. Na hapa ndipo jamii inapo pata taswira kuwa mambo ya urembo ni umalaya maana watoto/wasichana wakitoka huko wanajikuta tayari wameshaingia kwenye mazingira na hako katabia kanajijenga na kuwa ni kitu cha kawaida, "kama nilimvulia yule kwani huyu ana ubaya/tatizo gani gani".Wizara husika nikiamini ipo chini ya mwanamke mahiri itafanya kinachostahiki ili kukomesha tabia hizi ambazo pia zina athari kubwa ya kuwapotezea confidence wasichana wetu!
    Wadau tuliangalie hili kwa macho makali na roho zisizo na huruma kwa wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine kufanya uzembe uliopelekea hali hiyo!!!!

    ReplyDelete
  3. Yale yale na Lundenga na wenzie makambini? hawa jamaa wanajitia vidume sana.

    ReplyDelete
  4. Nimesoma habari yote hapo chini kwenye link,kama mshindi amepatikana kwa hila na ushahidi upo basi afutiliwe mbali, na kusiwe na mshindi mwaka huu 2013, maana huyo anaenda kututia aibu, pia na kuhakikisha kasoro hizi hazijitokezi mwakani.

    ReplyDelete
  5. Huyu mshindi lakini hapa anaonekana yuko airport, anaenda kwenye mashindano ya urembo ya dunia. Sasa wanaposema kuwa ikiwezekana kuwa alishinda kwa hila, avuliwe taji; sijui kama hapa akili imetumika. Maana akishamaliza kushiriki mashindano ya dunia, kutakuwa kumebaki nini??? Atashiriki, atashindwa, atarudi Tanzania. Hata mkimvua taji baadaye itakuwa haina maana

    ReplyDelete
  6. Sioni kwa nini huyo mtu apewe karipio kwa kosa la jinai ambalo hukumu yake ni kifungo cha maisha-kubaka na ushahidi mnao.Ninyi Basata ndio mnafuga wakosaji kwa kutoa karipio, karipio la nini ikiwa mtu amabaka, waliobakwa wapo na ushahidi upo?Pelekeni kesi mahakamani ikwa hamuwezi wapeni Legal and Human Righs Centre kazi ama NGOs wapeleke kesi mahali inapopaswa kwenda!

    ReplyDelete
  7. sawa kabisa,mshindi awe dsqualified,mwandaaji ashtakiwe na kufutiwa kibali.BASATA muwe serious, hii siyo issue ya karipio

    ReplyDelete
  8. Labda kuna mkuu pale BASATA amekamata ile kitu wanaita 10% ya zoezi zima.

    Teh teh, Tanzania bwana.

    ReplyDelete
  9. Hii ni tabia mbaya sana na udhalilishaji wa wanawake, na unyanyasaji. Tena ya kukemewa, wanawake lazima wawe Imara kwenye huu wakati wa udhalilishaji na unyanyasaji na ukandamizaji wa khaki zao. sio kunyanyasika, hafai kabisa huyo muandaji, na yasemwayo ni ukweli, uwezi kusema tu, kuna ukweli ndani yake

    ReplyDelete
  10. Mi hata siwaelewi

    ReplyDelete
  11. Yuko wapi yule mama wa kitengo fulani? Maana yeye hujifanya mkali sn lakini kwenye uzarilishaji kama huu yuko kimya kama hayupo vile,,kitengo ambacho kinamwandama waziri wetu mkuu eti tutampeleka mahakamani,,haya sasa tuwaone mkiwachukulia mashitaka hao wote waliowazarilisha madada zetu mm binafsi nimekeleka sn na hiki kitendo cha ajabu,,na mashindano haya kwanza hayana maana yoyote kwenye jamii yetu,

    ReplyDelete
  12. Waende shule wakasome..mabint wadogo wanataka utajiri na umaarufu wa chapchap ndio matokeo yake hayo mnalalamika nini sasa.Sisi tulioenda shule tulichapwa viboko,tukapigwa na umande na wakule kijijini tuliwashwa na upupu tukiwa maporini kutafuta kuni za walimu,sasa hawa wanaotaka kutoka fasta wacha wachapwe makofi na kungonolewa kilazima si wameyataka kwani aliitwa mtu hapo na kama hawakutaka kukamuliwa hao sio watoto wangegoma wasingesubiri mpaka utafiti ufanywe ndio waseme.
    Tuache kuiga upuuzi,hakuna nchi iliyoendelea duniani kupitia mashindano ya Umiss,Big brother wala Satr Search. Watu watilie umuhimu elimu tuache upuuzi huu.
    Uncle usibane kila mtu anahaki yakutoa maoni yake mradi sijatukana mtu.

    ReplyDelete
  13. Hizi tuhuma ni kweli kabisa, tena mengi hayajasemwa hapa, mimi ni boy friend wa mmoja wa washiriki, from her account of events, huyu jamaa hafai kuwa mwandaaji na wala hastahili kuaminiwa kulea mabinti coz aliwazalilisha sana, silaha yake kubwa ilikuwa ni kuwatoa self esteem kwa kuwatukana matusi ya nguoni constantly, inakuwaje mtu ambaye wasichana wanakuita baba then unawatukana kiasi hicho? Then from her account pia alikuwa anawalazimisha ngono, yaani anamwita msichana ucku kwenye room yake then anamthreat na kum solicit kwa ngono, kibaya zaidi ni kuwa jamaa inaaminika kaathirika na form her account alitembea na wasichana si chini ya wanne among them, mtu kama huyu ambae ana target a group of very vulnerable people, these are teenagers and young ladies who are trying to figure it out about their lives, then yeye ana distroy it all together, watu kama hawa wanastahili kushtakiwa na kufungwa jela iwe fundisho kwa wengine, wasichana wanaweza kuitwa na kutoa ushaidi sahihi kwa yote alowafanyia

    ReplyDelete
  14. Linda hakuna ulichosema ambacho haki-make sense

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...