Kikao cha dharura kilichoitishiwa usiku huu baina ya viongozi wa Yanga na kocha mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi kimemalizika huku kukiwa na usiri wa kilichojadiliwa na kuamuliwa.
Mwananchi limewashuhudia vigogo wa klabu hiyo wanaounda Kamati ya Utendaji, Rodgers Gumbo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na wajumbe wengine Alex Ngai, Yanga Makaga wakitoka katika ofisi za Rais wa klabu hiyo, Injinia Hersi Said.
Mbali na mabosi hao pia alikuwemo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Yanga, Andre Mtine lakini hakuna hata mmoja aliyetaka kuzungumzia lolote juu ya kilichojiri katika kikao hicho kizito, kilichoitishwa baada ya Yanga kufungwa mabao 3-1 na Tabora United kwenye Uwanja wa Azam Complex kikiwa ni kichapo cha pili mfululizo baada ya awali kulala kwa Azam Fc kwa bao 1-0. …...more
...more
Show less