Na Anthony John, Globu Jamii.
MKUU wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewataja baadhi ya Maafisa wa Jeshi la polisi wanao shirikiana na watu wanaojihusisha na uuzwaji wa dawa za kulevya.
Akizungumza na waandishi wa Habari mapema leo hii jijini hapa amesema Serikali ya awamu ya Tano haito vumilia vitendo vya uuzwaji wa dawa za kulevya na kutoa agizo kwa jeshi la polisi kuwakamata Maafisa wote wa jeshi la polisi waliotajwa kushirikiana na wauza madawa ya kulevya mpaka pale uchunguzi utakapo kamilika.
"nimepata taarifa kuwa baadhi ya Askari wa Jeshi polisi wanajihusisha na uuzwaji wa madawa ya kulevya na wengine wamekuwa na utaratibu wa kwenda kuchukua pesa kila jumamosi kwa wauzaji wa madawa ya kulevya na ndio maana biashara hii inaendelea kuwepo kwakuwa wanashirikiana na wauzaji" amesema Makonda.
Wakati huo huo Makonda amewataka wale wote waliotajwa kuhusika na kuuza dawa za kulevya wanatakiwa kufika katika kituo cha polisi kati kwaajili ya mahojiano.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akipitia orodha ya majina ya maafisa wa wanaotuhumiwa kujihusisha ya biashara ya madawa ya kulevya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...