Na Binagi Media Group
Taasisi ya AMI-TZ inajihusika na kilimo cha matunda na mbogamboga kama vile matikiti maji, nyanya, bamia, nyanya, pilipili mbuzi na aina nyinginezo nyingi.
Baada ya mavuno, taasisi hiyo hufanya usindikaji wa mazao kwa ajili ya kuwafikishia wateja wake majumbani, maofisini na mengine huuzwa moja kwa moja shambani.
"Baadhi ya vijana ukiwaeleza suala la kilimo wanakuona kama vile umepitwa na wakati lakini wale wanaojitambua wameingia kwenye kilimo na kinawalipa. Hivyo niwahamasishe watumie muda wao vizuri kwa kujishughulisha kwenye kilimo hivyo wasisubiri tu kazi za maofisini". Anasisitiza Deborah Mallaba, Mwanahabari na Mkurugenzi wa Taasisi ya AMI-TZ.
Mallaba anawasisitiza viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya Kata hadi Wilaya, kuongeza jitihasa za kuwakusanya vijana pamoja na kuwapatia mitaji ikiwemo pembejeo ili wajikite kwenye kilimo maana kilimo ni biashara na kinalipa ambapo pia hatua hio itasaidia kupunguza vijana mitaani.
"Napenda kuwaambia akina dada waamuke maana si vyema kuzurura tu wakisema hakuna ajira. Mfano mimi nimeanza kujiwekea kipato changu kupitia kilimo na nataka kuwa mafano bora kwa vijana wengine". Anasisitiza Aneth Shosha ambaye ni Afisa Masoko wa taasisi ya AMI-TZ huku akiwakaribisha vijana wengine kwenye taasisi hiyo ili wajifunze zaidi kuhusu kilimo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...