Rais Jakaya Kikwete akiongea na wachezaji wa timu ya mpira ya Taifa, Taifa Stars leo Ikulu jijini Dar es salaam alipokutana nao kuwapa hamasa waweze kupata ushindi katika mchezo wao dhidi ya Moroco utakaochezwa Juni 7, na michezo mingine ikiwa ni hatua ya kuiwezesha timu hiyo kukata tiketi ya kushiriki mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014.
Rais Jakaya Kikwete akiwaaga wachezaji wa Timu ya Taifa Stars mara baada ya kukutana nao leo Ikulu Jijini Dar es salaam kuwahamasisha washinde mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Moroco utakaofanyika June 7 ikiwa ni sehemu ya Taifa Stars kutafuta ticketi ya kucheza mashindano ya Kombe la Dunia.
Meneja wa Timu ya Taifa Stars Bw. Mukebesi akiteta jambo na Kepteni wa Timu ya Taifa Stars Juma Kaseja Ikulu jijini Dar es salaam walipokutana na Rais Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya Pamoja na wachezaji wa Timu ya Taifa , Taifa Stars, viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Taifa , Taifa Stars Ikulu jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Na. Veronica Kazimoto –MAELEZO.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amekutana na timu ya Taifa (Taifa stars) kwa lengo la kuitia moyo katika mechi ijayo kati yake na timu ya Moroco ikiwa ni harakati za Tanzania kutafuta tiketi ya kucheza fainali za kombe la Dunia kwa mara ya kwanza mwaka 2014.

Rais Kikwete ameiambia timu hiyo kuwa ina uwezo mkubwa wa kusonga mbele kutokana na uwezo mkubwa waliouonesha katika mchezo wao dhidi ya Gambia ambapo walifanikiwa kupata ushindi wa bao 2-0.

“Maadamu mara ya kwanza mliwashinda Gambia, hakikisheni pia mnapata ushindi dhidi ya Moroco, mkishinda tunafurahi sana na mkishindwa tunanyong’onyea sana,” amesema Rais Kikwete.

Aidha amempongeza kocha wa timu hiyo Kim Poulsen pamoja na Kamati ya Taifa ya ushindi ya Taifa stars kwa kuisaidia timu hiyo kiasi cha shilingi milioni 30 ikiwa ni mkakati wa kuiongezea nguvu kwa hatua iliyofikia na kuwataka wachezaji kujituma ili kuwafurahisha watanzania ambao hivi sasa wanaipenda timu yao ya Taifa.

Nae Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fenera Mukangara amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo nchini ili kuondoa changamoto zinazoikabili timu hiyo.

Kwa upande wake Kocha Poulsen, amemshukuru Rais Kikwete kwa kuwakaribisha na kuwatia moyo ambapo ameahidi kuifundisha vizuri timu hiyo ili kuhakikisha kuwa wanapata ushindi.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake kaptaini wa timu hiyo Juma Kaseja amemshukuru Rais Kikwete na kuahidi kujituma kwenye mazoezi na hatimaye kuibuka washindi kwenye mechi zijazo.

Taifa stars ambayo inakamata nafasi ya pili katika kundi C inatarajia kucheza ugenini na Morocco mnamo Juni 7 mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 23, 2013


    AMINIA DR DAU FUTNA YA SOKA UNAIJUA

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2013


    Hawa wachezaji wanatakiwa kupewa semina "elekezi" juu ya heshima kwa mkuu wa nchi. Kaseja na Msuva wanampa mkono Rais huku mkono mwengine (wa kushoto)upo mfukoni!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 23, 2013

    Haya ma ahadi yakizdi yanaongeza presha kwa wachezaji matokeo yake wanachemka

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2013

    "....to whom much is given,much is expected....".Msituangushe vijana.Wachapeni Morocco 2-0

    David V

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 24, 2013

    It will be interesting to see if they get to Brazil - Is it possible - I doubt!!!

    ReplyDelete
  6. Anony wa PILI nami nakuunga mkono nidhamu ni muhimu sana, anyway Bange mbaya jamani!

    ReplyDelete
  7. Mbona wachezaji wetu ni wafupi hivyo? haiwezi kuchangia kushindwa mara kwa mara? na Lishe naona kama nayo ni hafifu

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 24, 2013

    No.7 hapo juu naungana na wewe.

    Soka bila DISHI inakuwa mtihani, haiwezekani!

    Pana kila sababu Mahoteli yakatoa Mchango wa kugawa KUPONI za Wachezaji wa Taifa Stars kuweza kupata chakula angalau mlo mmoja wa uhakika kwa siku ili kujenga Afya zao.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 24, 2013

    Raisi Mhe. Dr. Jakaya Kikwete ni wakati sasa wa kugeukia ktk NDONDI ama KUFUKUZA MAJOGOO ama BAO LA KIZEE ama KUFUKUZA MBUZI!

    Kuliko kuwekeza ktk SOKA ambalo limetupotezea Fedha nyingi na muda bila matunda kuvuna!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 24, 2013

    Mdau wa Pili hapo juu.

    Wachezaji hao wawili ni Vijogoo inawezekana wakati huo walikuwa wapo ktk 7 UP yaani ''mambo yamewaharibikia'' huku Mhe. Raisi amekaribia hawakuona suluhisho kujisitiri bali watoe salamu Mkono mmoja huku mwingine ukiwa mfukoni!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 24, 2013

    Wanonekan kuchoka sana hao wakazanie msosi na wasivute bangi huondoa hamu ya kula

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 24, 2013

    Hivi jamani timu ya taifa mnakwenda Ikulu hamna hata Suit?

    Mnavaa mabango ya matangazo kila mahali jamani!

    Na nyie wadhamini hamuoni hata aibu kuwashinikiza wavae mabango hata Ikulu!

    nILISIKIA Sheria Ngowi atakuwa akiwatengenezea/kuwavalisha suit imeishia wapi?

    Mdau,
    Maseru, Lesotho

    ReplyDelete
  13. I'm very appreciative to the president for his continual support of the team. This is the only opportunity for Taifa Stars to show their true guts and prove to the president and Tanzanians at large that they deserve all this support.

    I can't wait longer for the show...go for it stars, beat them at their home like you did in Tanzania...God bless you lads

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...