Mtaalamu wa magonjwa ya moyo Dkt. Ferdinand Masau, amefariki dunia usiku wa kuamkia jana akiwa katika Hospitali ya Aga Khan, iliyopo Upanga jijini Dar es Salaama alikokuwa anatibiwa.
Habari hizo zimethibitishwa na marafiki wa karibu wa daktari huyo bingwa ambao hata hivyo hawakuwa tayari kutajwa majina kwa maelezo kuwa, wasemaji wa tukio hilo ni wanafamilia.
Maelezo kama hayo yalitolewa pia na mmoja wa maofisa wa hospitali ya Aga Khan, akisema wanafamilia ndio wanaoweza kuzungumzia taarifa za kifo cha mpendwa wao.
Enzi za uhai wake, baada ya kufanya kazi kwa miaka kadhaa nje ya nchi, alirejea nchini mwanzoni mwa miaka ya 2000 na kuanzisha taasisi ya moyo, akilenga kuwasaidia Watanzania wengi ambao kwa muda mrefu walikuwa wakikosa tiba ya uhakika nchini, hivyo kukimbilia nje ya nchi, hasa India.
Hata hivyo, ndoto zake ziliyumba kwa kiasi fulani kutokana na kukosa majengo ya uhakika kwa ajili ya taasisi yake, hivyo kulazimika kupanga katika majengo ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambako baada ya kudaiwa kushindwa kulipa kodi, mali zake ikiwa ni pamoja na vifaa na samani zote zilizokuwa katika taasisi hiyo zilipigwa mnada. Baadaye aliripotiwa kuibuka upya na kuanza kuwekeza taasisi nyingine ya magonjwa hayo eneo la Mbweni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
RIP fellow Dr, you can be proud that at least you tried to make a change in very difficult circumstances.
ReplyDeletePoleni sana familia ya marehemu. Utakumbukwa kwa kazi kubwa sana uliyoifanya wakati wa uhai wako.
ReplyDeletePamoja na vikwazo vyote alivyowekea na baadhi ya viongozi serikalini lakini subirini muone salamu za kinafiki zitakavyomiminika kwa kumpamba kwa sifa mbalimbali ilhali wakati wa enzi za uhai wake hawakumpa msaada wowote na wao ndio walikuwa mstari wa mbele kumkwamisha asitimize malengo yake ya kuwasaidia wanyonge wasiokuwa na uwezo wa kwenda India kutibiwa.Shame on them
ReplyDeletePoleni sana wanafamilia wa mpendwa wetu.
ReplyDeleteAlifanya alichoweza kuokoa maisha ya watanzania wasio na uwezo.mtu km huyu ndo anatakiwa kukumbukwa na tanzania I hope watatambua mchango wake ht baada ya kuondoka.rip unsang hero!
ReplyDeletesasa mtu mwema na mwenye malengo kama huyu anaondoka kabla ya kufikia malengo yake ya maana ktk jamii...mijitu ambayo haina mbele wala nyuma inaishi hadi miaka 100! watanzania kama tumelaaniwa hivi??
ReplyDeleteR.I.P Dr.
ReplyDeleteUlijitahidi kuonyesha kwamba hata bongo inawezekana tukatibu magonjwa yetu sisi wenyewe lakini ulikwamishwa na wachache wenye uchu wa pesa hata kama itagharimu uhai wa mtu!
shujaa halisi wa taifa...RIP
ReplyDeletePOLENI BANA BASU, MRUTUNGURU NA UK YOTE. KUMBE WATU WA KULETA MAENDELEO KISIWANI WAPO HAWASIKIKI TU.
ReplyDeleteSalute comrade! You fought the good fight of FAITH! May the Almighty God prepare happy dwellings for you in Heaven of Heavens! & May your name Dr Masau remind us of HOPE forever. Long live LOVE! Long live TIH! True work stands the test of time. Watanzania wenzangu, tumefiwa jamani, poleni.
ReplyDeleteMungu amrehemu Dr Masau.alikuwa mtu ambaye amejitolea kuisaidia jamii yetu.Nakumbuka jinsi alivyokuwa anasema hapati kuungwa mkono vya kutosha na serikali katika kuiendesha hospitali.Najua wanafiki (SERIKALI) watasema tumepoteza lulu.Lakini cha kujiuliza ,ni kwanini mtu kama huyu mwenye msaada mkubwa kama huu,alikuwa hapati kuungwa mkono vya kutosha na serikali??
ReplyDeleteNakumbuka katika moja ya mahojiano yake,Hayati Dr Masau,aliwahi kusema kwamba kuna magonjwa mengi ya moyo ambayo yalikuwa yanatibiwa na hospitali yake na kilikuwa hakuna ulazima wa serikali kutumia mamilioni kupeleka watu India.
Je lakini nani anajali???
Inahuzunisha sana jamani!!!!!!