Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ni taasisi iliyoundwa chini ya Sheria ya Chakula Dawa na Vipodozi Sura ya 219, ili kudhibiti ubora na usalama wa vyakula, dawa, vipodozi, na vifaa tiba kwa lengo la kulinda afya ya jamii dhidi ya madhara yatokanayo na matumizi ya bidhaa hizo.

Ili kutimiza wajibu huo, TFDA inasimamia pamoja na mambo mengine udhibiti wa uingizaji  wa vyakula kutoka nje ya nchi na utengenezaji wa vyakula ndani ya nchi kwa ajili ya kulinda afya za watumiaji. Katika udhibiti wa vyakula hivyo, michakato mbalimbali hufanywa ili kuwa na uhakika juu ya usalama wake kwa; kufanya tathmini na uchunguzi wa kimaabara, kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa usalama wa bidhaa kwenye soko na hatimaye kusajili majengo na vyakula baada ya kujiridhisha juu ya usalama wake.

Kutokana na mfumo wa udhibiti uliopo, Mamlaka imesajili bidhaa mbalimbali za vyakula vilivyofungashwa ikiwa ni pamoja na vinywaji aina ya soda zinazozalishwa nchini na zinazoingizwa kutoka nje.

Hivi karibuni kulitolewa taarifa na baadhi ya vyombo vya habari nchini kueleza kuwa kinywaji cha soda ni sumu. Mamlaka ina mashaka juu ya taarifa iliyotolewa kwa sababu haidhani kama ilitolewa kwa kuzingatia misingi ya kisayansi. TFDA inapenda kuwatoa hofu watumiaji wa kinywaji hiki kuwa, soda ni bidhaa ya chakula ambayo inatumika kote duniani na huzalishwa kwa kuzingatia viwango vya ubora na usalama. Kwa upande wa TFDA, soda zote zilizosajiliwa zimepitia katika mchakato ambao unatoa uhakika juu ya usalama wake kwa lengo la kulinda afya ya binadamu.

Tunapenda kutoa rai kwa vyombo vya habari kufanya utafiti wa kina hususan katika masuala yanayohusu ushahidi wa kisayansi ili kuondoa uwezekano wa kutoa taarifa kwa umma ambazo zinaweza kujenga hofu na mashaka ambayo hayastahili.

Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kupitia;
Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)
Barabara ya Mandela, Mabibo External,
S.L.P 77150
Dar Es Salaam, Tanzania
Simu:              +255 22 2450512/2450751/2452108
Fax:                 +255 22 2450793
Barua pepe:    info@tfda.or.tz
Tovuti:            www.tfda.or.tz

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hivi ni kwanini wagonjwa wa sukari hawapaswi kunywa soda?

    TFDA hamna budi kujibu hoja nzito kwa aya moja. Bila hata kutoa maelezo ya kisayansi kuonyesha kweli kinywaji cha soda ni salama kutuondolea hofu watumiaji

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 09, 2013

    Hii ndio shida kubwa ya waliopewa majukumu na dhima ya kusimamia mambo. Badala ya kujibu hoja, wanachofanya ni kutoa maneno matupu yasio na ushahidi wowote kama wale wanaowalaumu! Kutumiwa kwa soda duniani kote hakuifanyi kuwa salama. Haya si maelezo ya kitafiti wala kisayansi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 10, 2013

    Wadau wa wawili wa mwanzo mpo sahihi, hata mie nishangaa haya maelezo ya kukanusha mbona yapo juujuu tu pasipo ushahidi wowote wa kisayansi kama wao walivyonukuu sayansi hiyohiyo.Mimi nipo europe kitambo tu na taarifa hizi ni za kawaida sana na sijawahi kuona mamlaka za madawa na chakula zikitumia muda na fedha kukanusha taarifa kama hizi, Isitoshe ukitaka kuona ukweli wa taarifa hizi za vinywaji mbona zipo wazi tu ktk you tube na majaribio mengi tu yamefanywa ikiwemo la corrosive properties of drink like coca cola.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 10, 2013

    TPDF HIVI MNAJIELEWA, HALI HALISI INAJULIKANA KWAMBA VYAKULA VINGI AMBAVYO MUDA WAKE UMEPITA VINAUZWA MADUKANI HATA MADUKA MAKUBWA LAKINI HAKUNA HATUA YOYOTE MADHUBUTI AMBAYO MNACHUKUA ILI KUKOMESHA JAMBO HILI. SASA MNAPOAMBIWA KWAMBA SODA NI HATARI, NYINYI KAMA NDIO WAHUSIKA WAKUU, ILIKUWA NI WAJIBU WENU KUFANYA UTAFITI KAMA NYINYI, PALE MTAKAPOGUNDUA TATIZO TOENI TAHADHARI, KAMA VILE SIGARA UNAAMBIWA TUMIA LAKINI NI HATARI KWA HIYO NI JUKUMU LA MTUMIAJI KUTUMIA AU KUACHA. SIO MNACHUKULIA KIURAHISI RAHISI TUU KUTOA MAELEZO MAREFU OOH! DUNIANI KOTE KINYWAJI HIKI KINATUMIKA. TUMECHOKA NA NGONJERA. MARADHI YOTE MAKUBWA YAMEJAA TANZANIA, NA WANANCHI WENGI NI MASIKINI KUKABILIANA NA GHARAMA ZA MATIBABU, NGUVU KAZI INAZIDI KUTOWEKA! LENGO LENU NI NINI, WAPENI WANANCHI TAHADHARI!!! WATAAMUA WAO WENYEWE!

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousMay 10, 2013

      Mdau sio TPDF hao wanashughulika na ulinzi wa nchi bali ni TFDA

      Delete
  5. AnonymousMay 10, 2013

    Hizi ni akili za watanzania waliopewa mjukumu. Hivi, Tanzania hakuna muwajibikaji. Hebu ona majibu ya mtaalamu wa TFDA.Haya si maneno ya kuwaandikia wananchi. Huyu hapa analinda maslahi yake binafsi. Amesahau kuwa watoto wake, mama, bibi, babu wote hawa wanakunywa.

    Sisi tunataka utuhakikishie usalama, hatutaki longo longo.

    Kwa nfano: Tumeona nchini mwetu tualetewa vitu feki. na brand name zile zile kama ulaya lakini utakuta vinavyokuja kwetu ni faki. Na wasimamizi ni nyie hapo wataalam wetu. AIBU TUPU

    ReplyDelete
  6. Charles.May 10, 2013

    TFDA,
    Napongeza angalau kwa kuamka na kusema chochote ingawa hicho mlichosema!
    Hivi kweli mmeshindwa kusema au kutoa ufafanuzi wa sababu ambayo watu wanaitumia kusema kuwa soda ni sumu, nadhani hilo ndilo la msingi mlilopaswa kulijibu, na sio jibu hili mlilotoa ambalo kwa uelewa wangu mdogo ni jepesi saaaana!!
    watu hawasemi tu kuwa ni sumu kuna sababu, sasa nyie mmeshindwa kujibu hilo???!! nilitegemea labda baada ya kusema sio sumu kwa utafiti wenu wa kisayansi basi ingekuwa busara mkatoa huo utafiti wenu ulifanywaje, lini na nani waliohusika na findings zilikuwa zipi? ili tupate msingi wa pa kuanzia lkn kwa hili mlilotoa, naanza kuhoji utimamu wa aliyetoa taarifa hii toka TFDA.
    Asante!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 10, 2013

    Kaka Michuzi naomba unifikishie hili kwa hao TDFA, nakuomba kwa dhati ya moyo wangu,

    Kuna mchezo umezuka sasa hivi kwa vyakula ambavyo vinakaribia kuisha muda wake, au vimeshakwisha muda vinabadilishwa tarehe, wanafuta kwa kutmia utaalamu kwa mfano 2013, ile namba 3 inafutwa kwa juu kitaalamu nakuwekwa kama namba tano usipoangalia vizuri utadhani inaexpire 2015 kumbe ni 2013 na imeshaexpire kwa mfano April tunaomba uwaambie hao wanaoshabikia na kukalia umangi meza wapite super markets kufanya uchunguzi watagundua mengi sana, na watasaidia kupunguza cancers kwa kuwa vyakula vengine vinatumiwa na watoto. tunaomba utufikishie huu ujumbe !

    hatukatai vitu vinavokaribia kuisha muda wake kuchushwa bei, kinachostusha ni ile kubadilishwa tarehe!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 10, 2013

    TFDA imetoa taarifa kwamba soda ni salama na kwamba wanathibitisha kisayansi kupitia uchunguzi wa maabara sasa mdau ambaye anakataa maabara si sayansi atuambie ni nini. Naona wengi wanaobisha tayari wanataka majibu yaelemee wanakotaka. Tafiti hufanyika kila leo kokote katika wigo tofauti, je shirika la afya duniani (WHO) mbona halijasema soda ni tatizo, issue hapa ni kunywa kwa kiasi kwani kila kitu kikizidi kina madhara. BIG UP TFDA kwa kututoa wasiwasi, bebeni dhamana ya kutulinda

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...