![]() |
Dkt Hamisi Kigwangwalla |
Bungeni, Dodoma, Mei 1, 2013.
Napenda kutumia fursa hii kutoa taarifa kwa wanahabari na
umma kwa ujumla kufuatia habari iliyotoka leo mapema asubuhi kwenye gazeti la
Sauti ya watu Tanzania Daima, toleo Na.3071 na kuzua mjadala mkubwa na mzito
kwenye jamii pamoja na kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na hadhi, heshima
na uadilifu wangu kwenye jamii nikiwa kama kiongozi wa umma. Niwape pole wale
wote walioguswa na kushughulishwa na jambo hili, haswa familia yangu, ndugu,
marafiki na wananchi wa Nzega; ambao siku zote wanaamini sana katika uadilifu
wangu na namna ninavyosimamia misingi ya haki, sheria na uzalendo.
Nimesikitishwa sana na habari hii hususan kwa kuwa ilichapishwa bila kunipa
fursa ya kueleza kwa mapana uhusika wangu. Niwapongeze gazeti la Nipashe kwa kupuuza uzushi huu mara baada ya kunipigia na
kueleza upande wangu wa hadithi.
Kumekuwa na wimbi kubwa la baadhi ya watu kwenye baadhi ya
vyombo vya habari kuandika habari za uongo kwa maslahi maovu ya kuwachafua
wanasiasa na watu wengine. Watanzania sote tubadilike na tukatae tabia za
kutumika vibaya namna hii, maana ni hatari kwa ustawi wa weledi, na kwa umoja
na mshkamano wa kitaifa. Ukishaandika jambo ambalo litamchafua mwenziyo, hata
kama utamsafisha kiasi gani ni wazi hautokuwa na uhakika kuwa utawafikia wale
wale waliosoma zile za jana za kumchafua – hivyo ni jambo la kawaida kabisa
kuanza kwanza kwa kuwa na uhakika kabisa na habari kabla ya kuiandika.
Cry baby
ReplyDelete