Historia fupi ya Mtibwa

17 years ago | 3264 reads
Mtibwa Sugar Sports Club inayopatikana katika wilaya ya Mvomero takribani kilomota mia moja (100) kutoka Morogoro mjini ilianzishwa na wafanyakazi wa kiwanda cha sukari cha Mtibwa. Madhumuni ya awali ilikuwa kushiriki ligi katika ngazi ya wilaya na kutoa burudani kwa wafanyakazi. Mnamo mwaka 1989 timu ya mpira wa miguu ya mtibwa Sugar ilianza kushiriki ligi daraja la nne (4th division league) na kupanda ngazi kwa ngazi hadi daraja la kwanza mnamo mwaka 1996. Mashindano ya ligi daraja la kwanza yaliyobadilishwa jina na kuwa ligi kuu mwaka 1998. Kikosi cha mtibwa sugar kwa hivi sasa kinanolewa na mpashamisuli maarufu nchini, kocha mwenye jina kubwa katika medani ya mpira katika ukanda wa Afrika mashariki na kati Abdallah kibadeni “King Mputa” akisaidiwa na Patrick Mwangata

Drafti

Chemsha bongo Uswahili

Hebu tuone utalaam wako

Cheza hapa